Banner

Tuesday, July 31, 2012

2nd Semester examination results on >>>



Ifm Beaware






03/08/2012 - Declaration of 2nd Semester examinations for all 2011/2012 undergraduate and postgraduate programmes

HOSTEL APPLICATIONS FOR CERTIFICATE AND DIPLOMA STUDENTS (2012/2013)


HOSTEL APPLICATIONS FOR CERTIFICATE AND DIPLOMA STUDENTS (2012/2013)

1. I wish to inform Certificate and Diploma students that the Institute has some rooms for
student accommodation for academic year 2012/2013. The rooms will be provided to:
a) Students with special needs (physical disability or any serious health problem)
b) Students from upcountry on the basis of first come-first saved (as per available data)

2. There are only few spaces meant for Certificate and Diploma students, 300 beds in total.
Students who cannot get room at the campus will be assisted to get accommodation into
off-campus hostels which are recognized by the Institute.

3. Collect Hostel Application Form from Student Service Desk at Christian City Centre or
download it here.

4. Hostel fee for 2012/2013 is Tsh 400,000, paid with key deposit of 30,000, and 5,000 for
Student Hostel Identity Card. (Total Tshs 435,000)

5. Payment is made after your name is published in the list of successful hostel applicants.
List of successful hostel applicant will be posted on Institute website and notice board
one day after logging application form.

ISSUED BY OFFICE OF DEAN OF STUDENTS
27.07.2012

Tuesday, July 24, 2012

Wiki 1 baada ya kifo cha Mwenzetu Agnes,,, UDAKU



"""MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu Cha Usimamizi wa Fedha, (IFM) jijini Dar es Salaam, Agnes B. King’unza (pichani), amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuokotwa akiwa hajitambui katika ufukwe wa Bahari ya Hindi jirani na Coco Beach.
Habari za kipolisi zinasema Agnes alitekwa kisha akaokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali anatajwa kuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Coco Beach, ambako ndiko alikokutwa akiwa hajitambui.
“Polisi na hata watu wengine wanahisi kuwa msichana huyo alitekwa kisha kutupwa na watu wasiofahamika, baada ya kufanyiwa ukatili wa kutisha kwa kunyweshwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni sumu,” kilisema chanzo chetu cha habari ndani ya jeshi la polisi.
Habari zinasema baadaye mwanafunzi huyo ambaye alikuwa akichukua shahada ya mambo ya kodi, alipelekwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay kisha askari hao wakamkimbiza Hospitali ya Agha Khan kwa matibabu.
Hata hivyo, habari zinasema madaktari wa Agha Khan baada ya kuona hali ya mgonjwa ilikuwa mbaya, walimpa rufaa na kumpeleka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi na matibabu zaidi.
“Agnes alifariki jioni ya Julai 16, mwaka huu katika Hospitali ya Muhimbili na habari za kifo chake zilisababisha Chuo cha IFM kuzizima kwa wanafunzi kumlilia mwenzao,” kilisema chanzo hicho.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akasema kwamba wasamaria wema walisema waliona Bajaj ikifika eneo alilotupwa Agnes wakadhani wanatupa mzigo.
“Walipokwenda kuangalia wakakuta ni mtu akiwa hoi hajitambui. Baada ya kupelekwa hospitali siku ya pili alikuja mama mdogo wa marehemu Agnes aitwaye Veronica Galus na akaleta taarifa kuwa binti yao huyo amefariki dunia. Polisi tunaendelea na uchunguzi kuwatafuta wahusika,” alisema Kenyela. Hata hivyo, kifo hicho kimeacha maswali mengi kuwa binti huyo alilishwa nini na nani?
Mzazi wa marehemu aliyetajwa kwa jina la Bernad King’unza mkazi wa Kimara Dar, hakupatikana kwa maelezo kwamba alikuwa safarini Iringa kwenye mazishi ya mpendwa wao huyo yaliyofanyika nyumbani kwao Kalenga, Iringa Julai 19, mwaka huu."""

HABARI YOTE NI TOKA KWENYE GAZETI MOJA LA UDAKU AMBALO NINA WASIWASI NA UHAKIKA WAO JUU YA KIFO HIKI...

R.I.P AGNESS, MUNGU AKULAZE MAHALA PEMA PEPONI,,, AMINA!!!

Thursday, July 19, 2012

MSIBA WA MWANAFUNZI KUTOKA IFM: AGNES. B


Picture
Marehemu Agnes B. King'unza wakati wa uhai wake. Agnes alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mwaka wa kwanza akichukua Shahada ya Kodi (Bachelor of Taxation)
Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.

Marehemu Agnes B. King'unza alifariki Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mwili wa Marehemu Agnes King'unza umesafirishwa jana Jioni kwenda Nyumbani kwao Kalenga - Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika leo tarehe 19/07/2012.

Baba Padre wa Parokia ya Mbezi Temboni akibariki mwili wa Agnes King'unza
PictureMwili wa marehemu Agnes ukiwa kwenye jeneza ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwao Mbezi kwa Msuguri

Mwili wa Marehemu Agnes ukiwa kanisani tayari kwa
 heshima ya mwisho katika kanisa la Romani katoliki Mbezi Temboni

Makamu Rais wa Serikali ya wanafunzi wa IFM akitoa salamu
 za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake
Baadhi ya wanafunzi wenzake aliokuwa akisoma nao katika
 chuo cha usimamizi wa fedha IFM na kushoto mwenye shati la mistari
 ni mwakilishi kutoka wafanyakazi wa IFM

Friday, July 6, 2012

FACEBOOK PHONE

      





       

 Hii ni mahususi kwa FACEBOOKERS, ni "device" ya kipekee ambayo itakua inatumika ki"facebook" zaidi hii ni pamoja na kupiga picha na ku"upload" pamoja na mambo yote ambayo yanafanyika facebook. Yote hii ni kukurahisishia badala ya kuwa na simu ambayo masaa 23.5 upo nayo facebook basi unapata hiki kifaa ambacho ni moja kwa moja mpaka facebook bila kikomo... kinatumia "connection" za kawaida kama wi-fi au 3G yani unaweka chip ya mtandao wowote then mambo yanaendelea. Hapo ni ku"like" kwa kwenda mbele kama unavyoona ndio "button" pekee kwa juu, pembeni ni "button" ya camera.