Banner

Thursday, July 19, 2012

MSIBA WA MWANAFUNZI KUTOKA IFM: AGNES. B


Picture
Marehemu Agnes B. King'unza wakati wa uhai wake. Agnes alikuwa ni mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mwaka wa kwanza akichukua Shahada ya Kodi (Bachelor of Taxation)
Agnes aliokotwa na msamaria mmoja ambaye kwa taarifa za awali zinasema alikuwa ni mlinzi wa nyumba moja maeneo ya Koko Beach ambako ndio alikutwa ametupwa na watu wasiofahamika na kupelekwa kituo cha Polisi cha Oysterbay na baadae kukimbizwa hospitali ya Agha khan.

Marehemu Agnes B. King'unza alifariki Jioni ya tarehe 16/07/2012 katika Hospitali ya Muhimbili ambako alipelekwa baada ya Madaktari wa Hospitali ya Agha khan kushindwa kumtibu na kumrufaa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mwili wa Marehemu Agnes King'unza umesafirishwa jana Jioni kwenda Nyumbani kwao Kalenga - Iringa kwa mazishi ambayo yatafanyika leo tarehe 19/07/2012.

Baba Padre wa Parokia ya Mbezi Temboni akibariki mwili wa Agnes King'unza
PictureMwili wa marehemu Agnes ukiwa kwenye jeneza ulipokuwa ukiwasili nyumbani kwao Mbezi kwa Msuguri

Mwili wa Marehemu Agnes ukiwa kanisani tayari kwa
 heshima ya mwisho katika kanisa la Romani katoliki Mbezi Temboni

Makamu Rais wa Serikali ya wanafunzi wa IFM akitoa salamu
 za rambi rambi kwa niaba ya wanafunzi wenzake
Baadhi ya wanafunzi wenzake aliokuwa akisoma nao katika
 chuo cha usimamizi wa fedha IFM na kushoto mwenye shati la mistari
 ni mwakilishi kutoka wafanyakazi wa IFM

No comments:

Post a Comment