Banner

Saturday, May 12, 2012

TAMASHA LA MISS NA MR IFM KUHAIRISHWA MPAKA...

Lile tamasha la kuwania Miss na Mr IFM halikuweza kufanyika usiku wa leo kutokana na mvua kubwa iliyonyesha hapa jijini dar. Mvua hiyop iliyonyesha tangu asubuhi mpaka mida ya usiku ilipelekea kuhairishwa kwa hilo Tamasha, hii yote imekuwa "comfirmed" na MZEE WA VIMBWETA muda si mrefu baada ya kuongea na mmoja wa waandaaji wa tamasha aliyedai litafanyika baada ya wiki 2 ambapo ni baada ya TEST 2 za hapa IFM.

Kwa ujumla wanaomba radhi kwa usumbfu uliojitokeza kwani swala hilo liliukua nje saaaaana ya uwezo wao...
Hivyo U SHUD STAY TUNED  4 THE EVENT AFTER TEST 2.
HATIMAYE RAISI WA IFM 2012/2013 AMEPATIKANA

   Ikiwa ni shamra shamra kelele na vifijo usiku wa kuamkia tarehe 12/5/2012, ndipo alipatikana mshindi kati ya wagombea wawili pekee wenye UPINZANI mkubwa usio wa kawaida. Bwana MICHAEL, CHARLES na Bwana EMMANUEL KALINDAGA.
   Uchaguzi uliofanyika Ijumaa ya tarehe 11/5/2012 ndio ulitoa matokeo ya mshindi ambaye si mwingine bali ni MH. CHARLES MICHAEL.  Naye aliweza kumpiku mpinzani wake Bwana KALINDAGA (JEMBE) kwa kupata jumla ya kura 1600 wakati mwenzake akiambulia kura 1400. Matokeo hayo yalipokewa kwa shangwe na furaha kutoka kwa wafuasi wa MH. MICHAEL, wakati upande mwingine wakionyesha kutoridhika na matokeo ilihali wamezidiwa na kura takribani 200.
 
Hivyo kwa mwaka huu 2012/2013, IFM imemchagua CHARLES MICHAEL anayesoma Bachelor ya Insurance mwaka wa 2 kuwatumikia na kuwasimamia kwa uaminifu.

Wednesday, May 9, 2012

MISS na MR IFM 2012




   Hiyo kama inavyoonekana ni Miss IFM ambayo mwaka huu imekuwa ADVANCED kidogo mpaka na wakaka nasi tumepewa fursa na kwenye hicho kinyan'ganyiro cha u"MR".
Na si hapo pekee bali itakua inasindikizwa na shoo kali ya Msanii anayevuma na kutamba sana hapa Tanzania...DIAMOND PLATINUM atakayesababisha ndani ya viwanja vikali vya CINE Club. Na bila kumsahau Mshehereshaji wa siku hiyo si mwingine bali ni yuleee...MPOKI toka ZeComedy.

Mazee hiyo si ya kukosa yani ful kuwakilisha pande zile na 15000/= kwa wenye ID za IFM na 20000/= kwa maraia wengine...

USIKOSEEEEEEEE!!!

Uhandsome unampa urais CHARLES MICHAEL, IFM

Huyu ndie mgombea urais mwenye supporters wengi wasichana chuoni hapa wanaoonyesha dalili za kumpa ushindi, sababu ya msingi ya Bw.MICHAEL kumpita mwenzake sio sera tuu ni pamoja nakuwa "Handsome"

Upande mwingine tunae mgombea uraisi anayejulikana zaidi kama JEMBE, huyu ni Bwana KALINDAGA, EMMANUEL.  Naye ana wafuasi wengi walioweza kumpa kura na kupita katika uchaguzi wa mwanzo hapo Ijumaa tarehe 4/5/2012 na kuwa mpinzani pekee na mkubwa wa Bwana Michael.