Banner

Saturday, May 12, 2012

HATIMAYE RAISI WA IFM 2012/2013 AMEPATIKANA

   Ikiwa ni shamra shamra kelele na vifijo usiku wa kuamkia tarehe 12/5/2012, ndipo alipatikana mshindi kati ya wagombea wawili pekee wenye UPINZANI mkubwa usio wa kawaida. Bwana MICHAEL, CHARLES na Bwana EMMANUEL KALINDAGA.
   Uchaguzi uliofanyika Ijumaa ya tarehe 11/5/2012 ndio ulitoa matokeo ya mshindi ambaye si mwingine bali ni MH. CHARLES MICHAEL.  Naye aliweza kumpiku mpinzani wake Bwana KALINDAGA (JEMBE) kwa kupata jumla ya kura 1600 wakati mwenzake akiambulia kura 1400. Matokeo hayo yalipokewa kwa shangwe na furaha kutoka kwa wafuasi wa MH. MICHAEL, wakati upande mwingine wakionyesha kutoridhika na matokeo ilihali wamezidiwa na kura takribani 200.
 
Hivyo kwa mwaka huu 2012/2013, IFM imemchagua CHARLES MICHAEL anayesoma Bachelor ya Insurance mwaka wa 2 kuwatumikia na kuwasimamia kwa uaminifu.

No comments:

Post a Comment